Showing posts with label Kuitwa Kazini. Show all posts
Showing posts with label Kuitwa Kazini. Show all posts

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI




Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013 waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi baada ya usaili kukamilika


Angalia orodha ifuatayo:Orodha ya kuitwa chuoni moshi 2014
Maelekezo Muhimu.
Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.
Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.
Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.
Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
Chandarua chenye upana futi tatu
Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
Pasi ya Mkaa
Ndoo moja
Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).
Pesa kidogo ya kujikimu.
Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.
Angalia orodha ifuatayo:Orodha ya kuitwa chuoni moshi 2014

KUITWA KAZINI UTUMISHI AUGUST - 2014 - Placements


KUITWA KAZINI UTUMISHI  AUGUST - 2014 - Placements

Kuitwa kazini kwa waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 08 Julai hadi 09 Agosti, 2014 

Tafadhali bonyeza hapo link hapo chini kuona majina yote.

KUITWA KAZINI-23-AUGUST-2014 (Placements)

Usaili wa Jeshi la Polisi Tanzania - Mbeya



Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.

Muhimu:

Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.
Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s) ], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa.
Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI 01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.

KUITWA KWENYE USAILI JESHI LA POLISI TANZANIA




Kuitwa kwenye Usahili:Orodha ya vijana wa kidato cha Sita na Nne waliochaguliwa
Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013 na kidato cha sita mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya kujiunga na Jeshi la Polisi.
Usaili utafanyika katika miji ya makao makuu ya mikoa Tanzania Bara Kwa tarehe zilizooneshwa kwenye jedwali hapa chini:



NA
MIKOA
KITUO CHA USAILI
TAREHE ZA USAILI
MUDA WA USAILI

1
TANGA
OFISI YA RPC TANGA
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

2
PWANI
OFISI YA RPC PWANI
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

3
DSM ZONE
OFISI YA RPC ILALA,KINONDONI,TEMEKE
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

4
MTWARA
OFISI YA RPC MTWARA
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

5
LINDI
OFISI YA RPC LINDI
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

6
SIMIYU
OFISI YA RPC SIMIYU
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

7
SHINYANGA
OFISI YA RPC SHINYANGA
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

8
TABORA
OFISI YA RPC TABORA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

9
KATAVI
OFISI YA RPC KATAVI
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

10
RUKWA
OFISI YA RPC RUKWA
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

11
KILIMANJARO
OFISI YA RPC KILIMANJARO
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

12
ARUSHA
OFISI YA RPC ARUSHA
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

13
MANYARA
OFISI YA RPC MANAYARA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

14
SINGIDA
OFISI YA RPC SINGIDA
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

15
DODOMA
OFISI YA RPC DODMA
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

16
KIGOMA
OFISI YA RPC KIGOMA
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

17
MWANZA
OFISI YA RPC MWANZA
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

18
MARA
OFISI YA RPC MARA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

19
GEITA
OFISI YA RPC GEITA
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

20
KAGERA
OFISI YA RPC KAGERA
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

21
MOROGORO
OFISI YA RPC MOROGORO
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

22
IRINGA
OFISI YA RPC IRINGA
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

23
MBEYA
OFISI YA RPC MBEYA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

24
NJOMBE
OFISI YA RPC NJOMBE
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

25
RUVUMA
OFISI YA RPC RUVUMA
08-11 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

Muhimu:
(i) Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitashughulikia usaili wa mtu ambaye hayupo kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili.
(ii) Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)] na nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate)]. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
(iii) Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..
(iv) Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.
PAKUA ORODHA YA MAJINA
1.Orodha ya vijana wa kidato cha Sita waliochaguliwa kufanya usahili
2.Orodha ya vijana wa kidato cha Nne waliochaguliwa kufanya usahili

KUITWA KAZINI - ZIMAMOTO NA UOKOAJI - 5/5/2014

KUITWA KAZINI KWA WALIOFAULU INTERVIEW PCCB , APRILI 2014




Kufuatia usaili (Oral Interview) uliofanyika kati ya tarehe 03/02/2014 – 14/03/2014 TAKUKURU Makao Makuu kwa watahiniwa walioomba nafasi za Afisa Uchunguzi daraja la pili na wachunguzi Wasaidizi, 
yafuatayo ni matokeo ya usaili huo:
users online